Kombamwiko alikuwa akiishi kwa raha mustarehe na wazazi wake kijijini. Ngoja basi siku moja akutane na Faragano, mende mmoja mjuaji, ambaye alimsifia Kombamwiko kuhusu maisha matamu ya mjini, kulingana na yale ya 'kijinga' ya kijijini kwao. Hadi Kombamwiko akaamua kwenda huko mjini akajionee mwenyewe uhondo, dhidi ya pingamizi za wazazi wake. Safari ikaanza. Kumbe, lahaula! Mambo sivyo kama alivyotarajia! Walikumbwa na visa na mikasa; wakateseka vilivyo na mwishowe wakaamua heri warejee nyumbani; kwani mwenda tezi na omo, marejeo ni ngamani.Hadithi hii ya kuvutia inasimulia visa vya safari hiyo ya Kombamwiko na wenzake.
show more